Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

23 JULAI 2020

23 JULAI 2020

Pakua

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameuambia ulimwengu wa nchi za Kiarabu kwamba sasa ni wakati wa kugeuza janga la virusi vya Corona au coronavirus">COVID-19 kuwa fursa ya kujijenga upya na kwa ubora zaidi. Watoto zaidi ya 32 wamepoteza au kutenganishwa na mzazi mmoja au wote kutokana na Ebola tangu kuzuka kwa mlipuko mpya Juni Mosi kwenye jimbo la Equateur Magharibi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC,limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. Nchini Yemen, vita vya wenyewe kwa wenyewe na janga la ugonjwa wa virusi vya Corona, au coronavirus">COVID-19, vimeleta taabu kwa wananchi huku familia zikihaha kujinusuru na Umoja wa Mataifa ukiingilia kati kusaidia.

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
12'51"