Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mustakbali wa wanafunzi wakimbizi wamulikwa kati ya changamoto ya COVID-19, Uganda

Mustakbali wa wanafunzi wakimbizi wamulikwa kati ya changamoto ya COVID-19, Uganda

Pakua

Baadhi ya hatua zilizochukuliwa na nchi nyingi duniani kama sehemu ya njia za kudhibiti kuenea kwa COVID-19, zimeathiri vibaya Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs likiwemo lile namba nne linalochagiza fursa za elimu bora. Nchini Uganda, kufungwa kwa taasisi za elimu ni miongoni mwa hatua za kwanza kabisa kuchukuliwa na hatimaye kuathiri moja kwa moja wanafunzi zaidi ya milioni 15. Hata hivyo serikali imetumia mbinu mbalimbali ikiwemo kusambaza masomo kupitia matangazo ya redio na televisheni ambavyo havijaweza kuwafikia wote. Katika kambi ya wakimbizi ya Kyangwali nchini humo, wanafunzi wakisaidiwa na walimu na wanajamii, wamechukua hatua ya kuelimishana ili muda huo wenye changamoto nyingi kambini usipotee na kufifisha ndoto zao. Je, wanafanya nini?

Ungana na John Kibego katika sehemu ya kwanza ya mahojiano na wanafunzi; Feza Kabera na Shamil Bao Yahaya wakiwa katika kambi ya wakimbizi ya Kyangwali.

Audio Credit
Assumpta Massoi/John kibego
Audio Duration
3'57"
Photo Credit
UN/ John Kibego