UPU na usongeshaji wa posta kidijitali duniani
Ukuaji wa Kiuchumi
Teknolojia ya kidijitali inavyosonga, vivyo hivyo huduma za posta duniani, lengo ni kuhakikisha kuwa posta inakwenda na wakati. Shirika la Umoja wa Mataifa la huduma za posta duniani, UPU linachukua hatua kuona kuwa lenyewe linakuwa kichocheo kwa nchi wanachama kuwa na huduma za posta zinazokwenda na wakati hasa zama za sasa za kidijitali. Mkurugenzi wa Maendeleo ya Ushirikiano kutoka shirika hilo, Mutua Muthusi anazungumza na Evarist Mapesa wa Idhaa hii na anaanza kwa kuelezea hali ya huduma ya posta hususan katika nchi zinazoendelea au maskini katika zama za sasa za maendeleo ya kidijitali. Mahojiano haya yamefanikishwa na Kayla Redstone wa UPU.