MONUSCO tuko bega kwa bega na CENI DRC
Haki za binadamu
Tayari Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo amethibitisha uchaguzi mkuu utafanyika nchini humo mwishoni mwa mwaka huu kama ilivyopangwa. Sasa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO unaeleza ni hatua gani zimefanyika na zinafanyika ili kuhakikisha uchaguzi huo unakuwa huru,a wahaki na unafanyika kwa amani.