Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

28 FEBRUARI 2024

28 FEBRUARI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia msaada wa chakula nchini Sudan, na ulinzi wa amani katika jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini amabapo idadi ya wakimbizi imeongezeka. Makala tunakupeleka nchini Rwanda na mashinani nchini Kenya, kulikoni?  

  1. Msaada wa chakula cha dharura uliotolewa na Ukraine kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP kwa ajili ya operesheni zake nchini Sudan, leo umewasili katika bandari ya Port Sudan na kuapakiwa Kwenye malori tayari kwa kuwasambazia mamilioni ya watu wenye uhitaji wa haraka.
  2. Huku mzozo wa Sudan ukiendelea, wakimbizi na wanaorejea wanamiminika katika mipaka ya nchi jirani ya Sudan Kusini, wengi wamekuwa wakitafuta hifadhi katika jimbo la Upper Nile nchini humo na wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu.  Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS umefanya mazungumzo na uongozi wa jimbo hilo kuona namna ya kuwasaidia. 
  3. Makala tunaangazia chanjo kwa watoto nchini Rwanda ambako Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linaifadhili Rwanda Biomedical Centre (RBC) ambalo ni shirika kuu la kitaifa la utekelezaji wa afya lenye jukumu la kufanya utafiti wa kisayansi, kutoa huduma za uchunguzi, na kutekeleza afua za kiafya ili kulinda taifa la Rwanda dhidi ya magonjwa na matishio mengine ya kiafya.
  4. Na mashinani tutaelekea nchini Kenya kusikia ujumbe wa mfugaji kuhusu uwekezaji katika sekta ya uzalishaji wa mifugo unaowezeshwa na Benki ya Dunia.

Mwenyeji wako ni Evarist Mapesa, karibu!

Audio Credit
Leah Mushi
Sauti
11'18"