07 MEI 2020

7 Mei 2020

Katika Jarifda la Habari hii leo kwenye Umoja wa Mataifa Flora Nducha anakuletea

-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF lasema takribani watoto milioni 116 watazaliwa wiki 40 baada ya kutangazwa rasmi kuwa janga la corona limekuwa janga la kimataifa mnano mwezi Machi makwa huu

- Ripoti mpya iliyotolewa leo na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya madawa na uhalifu UNODC imesema janga la COVID-19 limeingilia utaratibu wa kusafirisha mihadarati kwa njia ya anga na kuwafanya wafanyabiashara wa bidhaa hizo haramu kusaka njia mbadala

-Nchini Niger mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF unashirikisha machifu na wananchi katika kupiga vita janga la COVID-19

-Makala yetu leo inatupeleka Uganda kumulika harakati za kusaka tiba ya COVID-19 , hudu mitishamba ikipatiwa nafasi

-Na mashinani tunakwenda Congo DRC utamsikia binti ambaye anahisi janga la corona linataka kukatisha ndoto zake lakini hakati tamaa.

Audio Credit:
UN News/Flora Nducha
Audio Duration:
12'

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud