Vituo vya wahamiaji Niger vimejaa pomoni, IOM yataka hatua za dharura
Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, (IOM) linatoa wito kwa kuanzishwa kwa haraka njia ya dharura ya kiutu kutoka Niger ili kupunguza mlundikano kwenye vituo vyake vya mpito nchini humo ambako maelfu ya wahamiaji wamepata hifadhi, wengi wao wakisubiri kurejea nyumbani.