COVID-19

Mtanzania atengeneza mashine ya Oksijeni ambayo haina ulazima kuwa na mtungi wa gesi

George Nyahende, raia wa Tanzania amebuni na kutengeneza mashine ya oksijeni ambayo ina sifa za kipekee ambazo anasema zinatokana na mazingira hususani ya vijiji vya Tanzania.

Unyonyeshe vipi mtoto wakati wa COVID-19? Pata Mwongozo wa UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limetoa mwongozo wa unyonyeshaji mtoto salama wakati huu dunia inakabiliana na janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19 na kutoa maelekezo ya kumlisha mtoto kwa kufuata mwongozo huo.

Maziwa ya mama mwenye COVID-19 bado ni salama kwa mwanae- UNICEF

Makampuni ya kuuza vyakula vya watoto yatakiwa kuzingaia sheria za masoko na kutosambaza taarifa za upotoshaji

2 Agosti 2021

Jaridani leo Jumatatu Agosti 2, 2021

Sauti -
10'50"

Kasi ya kupeleka chanjo za COVID-19 barani Afrika yaongezeka

Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO, kanda ya Afrika limesema sasa kuna kasi kubwa ya kupeleka shehena za chanjo dhidi ya ugonjwa wa Corona au COVID-19 barani Afrika, wakati huu ambao bara hilo limeshuhudia wiki ya pili ya ongezeko kubwa la maambukizi ya ugonjwa huo.

Julai 29, 2021

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani,

Sauti -
12'23"

Anayepinga Corona aulize koo zilizokumbwa na janga- Rais Samia

Hii leo huko nchini Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan amezindua kazi ya utoaji wa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Corona au COVID-19 kwa yeye mwenyewe kupatiwa chanjo hiyo pamoja na viongozi wengine waandamizi wa serikali, huku akisisitiza juu ya usalama wa chanjo hiyo  iliyowasili nchini humo mwishoni mwa wiki kupitia mpango wa Umoja wa Mataifa wa kusaka chanjo, COVAX.

28 Julai 2021

Jaridani Jumatano 28, 2021 

Hii leo huko nchini Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan amezindua kazi ya utoaji wa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Corona au COVID-19.

Sauti -
13'41"

Tusijidanganye, wimbi la tatu la Covid-19 Afrika halijaisha kabisa - WHO

Baada ya wiki nane mfululizo za kuongezeka kwa kasi ya maambukizi, sasa maambukizi mapya ya  Covid-19 barani Afrika yamepungua kasi, Afrika Kusini ambayo ndiyo ilikuwa na idadi kubwa ya maambukizi ikishuhudia kushuka kwa kasi kwa maambukizi mapya ingawa maendeleo haya yanaweza kuwa ya muda mfupi, takwimu mpya kutoka kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, WHO zimeonesha. 

Covid-19 imeathiri kazi yangu ya ualimu na sasa ninauza juisi – Mwalimu Catherine Tuhaise 

Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na kutangazwa na shirika la kazi la Umoja wa Mataifa

Sauti -
3'44"