Wanawake lazima wapewe kipaumbele kutimiza ajenda ya 2030

23 Januari 2018

Mashirika ya misaada ya kibinadamu, asasi za kiraia na serikali mbalimbali zimehimizwa kuwekeza nguvu zao katika kuinuwa vipato vya watu vijijini hususani wanawake kwa kupitia miradi ya ujasiriamali ,kutoa  mafunzo, semina na mbinu mbalimbali zitakazoliwezesha kundi hilo katika jamii.

Kwa kulitambua hilo huko nchini Pakistan  shirika la kazi duniani ILO kwa ushirikiano na serikali ya Canada wameanzisha kampeni ya usawa kijinsia kwa wanawake vijijini kwa kutoa elimu na mafunzo  ya ujasiriamali ili waweze kujikwamua na umasikini. Nini  kilichojiri huko? Ungana na Patrick Newman katika Makala hii upate undani…

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud