Chuja:

Pakistan

Familia zinaishi bila makazi baada ya kuhamia eneo salama huku maji ya mafuriko yakikumba vijiji vya mkoa wa Balochistan nchini Pakistan.
© UNICEF/A. Sami Malik

WHO yasafirisha kwa ndege vifaa vya matibabu hadi Pakistan

Shehena mbili zilizobeba vifaa vya matibabu na vifaa vingine muhimu vinavyohitajika sana zimewasili Karachi, Pakistani, leo ili kukabiliana na uhaba mkubwa nchini humo baada ya uharibifu uliofanywa na mafuriko makubwa zaidi katika historia ya hivi karibuni. Shehena hizo zina tani 15.6 za vifaa kwa ajili ya kipindupindu, maji na mahema ya matumizi mbalimbali ambayo yanaweza kutumika kama mahema ya matibabu.

30 AGOSTI 2022

Katika jarida la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea 

-Nusu ya vituo vya huduma za afya duniani kote vinakosa huduma za usafi na hivyo kuwaweka wagonjwa na wahudumu wa afya katika hatari kubwa ya kusambaza magonjwa na maambukizi kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa leo na WHO na UNICEF.

Sauti
12'56"
Mtoto akipatiwa chanjo dhidi ya polio huko Cotonou nchini Benin
©Yézaël Adoukonou/ Nations Unies Bénin

COVID-19 yarudisha nyuma utoaji chanjo kwa watoto kwa miongo mitatu

Licha ya mwaka 2021 kutegemewa utakuwa mwaka bora wa utoaji chanjo kwa watoto wachanga baada ya janga la COVID-19 kuvuruga utoaji chanjo mwaka 2019 na 2020, ripoti iliyotolewa leo na Umoja wa Mataifa imeonyesha kiwango cha utoaji chanjo duniani kimeendelea kupungua maradufu na kurudisha takwimu kwa miongo mitatu nyuma huku watoto milioni 25 wakikosa chanjo muhimu za kuokoa maisha yao.

Sauti
2'51"