Wafanyakazi wa kujitolea UM wana mchango mkubwa katika jamii
Leo ni siku ya kimataifa ya kujitolea ambayo kila mwaka huwa Desemba 5, kauli mbiu mwaka huu ni “jitolee chukua hatua kwanza”
Ni kijana Hussain Salim mratibu wa miradi na matukio kutoka Rally Tanzania Society, taasisi isiyo ya kiserikali inayohusika na shughuli za kujitolea na inafanya kazi kwa karibu na Umoja wa Mataifa nchini humo katika kusongesha mbele malengo ya maendeleo endelevu SDGs.
Umoja wa Mataifa unasema maelfu ya wafanyakazi wake wa kujitolea kama kijana Hussein wana mchango mkubwa, katika kusaidia kufanikisha ajenda ya umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu ya 2030 lakini pia malengo ya jamii wanakojitolea. Hussein ana ujumbe
(Sauti ya Hussain Salim)

Kwa mujibu wa Stuart J. Moran meneja wa mpango wa kujitolea wa Umoja wa Mataifa Darfur bila mchango wao kibarua kingekuwa kigumu.
(Sauti ya Stuart J. Moran)
"Watu wetu wa kujitolea wana jukumu muhimu sana la kusaidia jukumu kubwa la mpango wetu ambalo ni kulinda raia, hivyo tunapoona doria za UNAMID, helkopta na kadhalika, vitu hivi haviwezi kufanyika bila msaada wa mfumo wa mfumo wa mpango wetu ikiwemo wafanyakazi wa kujitolea wa umoja wa Mataifa. "