Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kiswahili: Juhudi binafsi za kukiendeleza sambamba na kinavyoleta ahueni kwa walioko kwenye mizozo

Kiswahili: Juhudi binafsi za kukiendeleza sambamba na kinavyoleta ahueni kwa walioko kwenye mizozo

Pakua
Zaidi ya mwezi sasa umepita tangu maadhimisho ya kwanza ya lugha ya Kiswahili duniani na harakati zinaendelea kusongesha lugha hiyo adhimu. Ni katika nyakati kama hizo watu wanaanza kutambua umuhimu wa lugha yoyote katika maendeleo na hadi kupatiwa hadhi ya kimataifa inakuwa juhudi nyingi zimefanyika. Ziko juhudi binafsi, za kikanda na za kimataifa ambazo zinawezesha lugha kutumika hata pale penye mazingira magumu ili kuleta ahueni kwa wenyeji. Mathalni huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kuna mizozo na wageni wanaozungumza kiswahili wanapata ahueni pale wenyeji wanaokwenda kuwanyooshea mkono wanazungumza pia lugha hiyo na ndivyo inavyodhihirika kwenye makala hii sambamba na juhudi binafsi za wananchi kusongesha kiswahili akiwemo John Jackson, mtanzania anayeishi Ujerumani. Katika makala hii tutasikia pande zote na hapa Thelma Mwadzaya anasimulia makala hii na Meja Doreen Arcad Mchomba, mtaalamu wa masuala ya saikolojia katika kikosi cha 9 cha Tanzania, kwenye ujumbe wa Umoja wa Matiafa wa kulinda amani nchini DRC, MONUSCO. Meja Mchomba anaanza kwa kuelezea sababu ya kupenda lugha ya Kiswahili.
Audio Credit
Anold Kayanda/ Thelma Mwadzaya
Sauti
4'8"
Photo Credit
MONUSCO/TANZBATT_9