Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Asante UNDP Tanzania sasa wanawake Kigoma tunaona matunda ya kuweko kwenye vikundi

Asante UNDP Tanzania sasa wanawake Kigoma tunaona matunda ya kuweko kwenye vikundi

Pakua

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo duniani, UNDP limejizatiti kusaidia mipango ya kuinua wanawake na vijana kwa  kupatia makundi hayo mitaji. Hilo linafanyika mkoani Kigoma nchini Tanzania ambako uweko wa wakimbizi ulibainika kuleta changamoto katika upatikanaji wa  mahitaji siyo tu kwa wakimbizi bali pia kwa jamii za wenyeji ambao wanawapatia hifadhi. Kupitia mradi wa pamoja wa Kigoma, KJP unaotekelezwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo UNDP, wakazi wa wilaya za Kakonko, Kasulu, na Kibondo wameona matunda ya UNDP kwani wamepatiwa si tu mitaji bali pia stadi za kuendesha vikundi na miradi yao. Makala hii iliyofanikishwa na UNDP inafafanua zaidi na msimulizi wako ni Leah Mushi.
 

Audio Credit
Assumpta Massoi/Leah Mushi
Audio Duration
4'46"
Photo Credit
UN News/Assumpta Massoi