Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chukua hatua zifuatazo kuepusha sumu kuvu kwenye mazao

Chukua hatua zifuatazo kuepusha sumu kuvu kwenye mazao

Pakua

Umoja wa Mataifa kupitia mashirika yake ikiwemo lile la chakula na kilimo, FAO pamoja na lile la afya duniani, WHO yanapigia chepuo umuhimu wa kukabiliana na sumu kuvu kwenye mazao. Hii ni kwa kutambua kuwa sumu kuvu sio tu ina madhara kwa afya ya binadamu bali pia ni moja ya sababu kubwa ya upotevu wa mavuno ya mazao. Uhifadhi duni wa mazao kama vile mahindi, karanga husababisha mazao hayo kupata sumu kuvu na hivyo yasiweze kuuzika na pia iwapo mtu atanunua na kula basi anaweza kupata madhara ya kiafya. Je sumu kuvu ni nini? Hiyo ni sehemu ya makala yetu kwa leo kutoka huko Morogoro nchini Tanzania ambako Hamad Rashid wa Radio washirika MVIWATA FM amezungumza na wataalamu ambao pia wanatoa ushauri kwa wakulima wa nini kifanyike kukabiliana na tatizo hilo.

Audio Credit
Leah Mushi/ Hamad Rashid
Audio Duration
3'26"
Photo Credit
FAO