Mafuriko Nigeria yaathiri zaidi ya watu milioni 3 na kukatili maisha ya watu 600: OCHA
Mafuriko makubwa yanayoikumba Ningeria hivi sasa hayajawahi kushuhudiwa kwa zaidi ya muongo mmoja limesema Ofisi ya Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA na kuongeza kuwa hadi kufikia sasa zaidi ya watu milioni 3 wameathirika wengine wakipoteza maisha, zaidi ya milioni kutawanywa na miundombinu muhimu ikiwemo nyumba, barabara na mashamba vimesambaratishwa.