Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wazazi tulinde watoto wetu dhidi ya mimba katika umri mdogo - Catherine Kobusinge Kamanyire

Wazazi tulinde watoto wetu dhidi ya mimba katika umri mdogo - Catherine Kobusinge Kamanyire

Pakua

Nchini Uganda ripoti kutoka wilaya mbalimbali zinaonesha ongezeko la idadi ya wasichana waopata mimba utotoni kuliko wakati wowote kabla ya shule kufungwa kutokana na COVID-19. Wakati wilaya ya Hoima pekee imeripoti mimba za utotoni zaidi ya 6,000 wilaya jirani ya Masindi imeripoti zaidi ya wasichana 1,500 waliopata mimba kati ya mwezi Januari na Juni mwaka huu.

Uganda ina takribani wilaya 135.

Kwa kuitikia ripoti hizo za kusitua, mwandishi wetu wa Uganda John Kibego amezungumza na Mkurugenzi wa shirika la kupigania haki za watoto na wanawake la HONECRIC, Bi. Catherine Kobusinge Kamanyire ambaye anatoa mawaidha kuhusu ulinzi wa watoto na vilevile kuwatia moyo wazazi akisema hata baada ya mimba ya utotoni, matumaini yanasalia. 


(Makala ya John Kibego)
 

Audio Credit
John Kibego
Audio Duration
3'53"
Photo Credit
© UNFPA Myanmar/Yenny Gamming