Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunaandaa mashindano mbalimbali ya michezo ili kuwaondoa vijana kwenye mawazo mabaya - ETCO

Tunaandaa mashindano mbalimbali ya michezo ili kuwaondoa vijana kwenye mawazo mabaya - ETCO

Pakua

Mara kwa mara Umoja wa Mataifa umeendelea kusisitiza kuwa vipaji vikiwemo vya michezo vina mchango mkubwa katika kusaidia kuleta maendeleo na amani.

Vijana wanapotambuliwa vipawa vyao wanapata shughuli rasmi za kufanya na hivyo kuinua vipato vyao, kuwaondoa katika mazingira hatarishi na faida nyingine za ujumla ambazo muunganiko wake unasaidia kuelekea katika kutimiza malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.

Mwandishi wetu wa Kenya Jason Nyakundi amezungumza na Collince Onyango, muasisi wa mradi unajulikana kama ETCO au Empowering the Community, ambao lengo lake ni kutambua vipawa miongoni mwa vijana wasiokuwa na ajira mtaani Kibera mjini Nairobi na kisha kuwaunganisha na watu au mashirika yatakayowapa ajira.   

 

Audio Credit
Jason Nyakundi
Audio Duration
3'7"
Photo Credit
© UN-Habitat /Julius Mwelu