Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNDP na TAHA nchini Tanzania wajenga vituo vitano vya kuhifadhi na kufungasha mazao

UNDP na TAHA nchini Tanzania wajenga vituo vitano vya kuhifadhi na kufungasha mazao

Pakua

Umoja wa Mataifa unapigia chepuo mifumo sahihi ya chakula inayolenga kuongeza mnyororo wa thamani kuanzia shambani hadi kwa mlaji. Hatua hii siyo tu inasaidia kutokomeza njaa bali pia inaongeza kipato kwa mkulima na ustawi kwa mlaji kwa kuwa zao ambalo linapatikana eneo moja la dunia linaweza kusafirishwa katika ubora wake na kufikia eneo lingine la dunia katika ubora huo huo.

Ni kwa kuzingatia hilo nchini Tanzania, shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo duniani, UNDP limeunga mkono hatua za chama cha wakulima wa mboga na matunda, TAHA kwa kusaidia ujenzi wa vituo vitano vya kuhifadhi na kufungasha mazao mbalimbali na sasa matokeo yameshaanza kuwa wazi.

Ni kwa vipi basi? Ungana na Anold Kayanda katika makala hii.

 

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
7'56"
Photo Credit
TAHA