Nchini Kenya vijana wabuni kifaa cha kunawa mikono kwa urahisi kujikinga na virusi vya Corona
Leo ni siku ya kimataifa ya vijana kaulimbiu mwaka huu ikiwa "ujumuishwaji wa vijana kwa ajili ya hatua za kimataifa" Umoja wa Mataifa ukisisitiza kuwa kundi hilo la watu katika jamii linaweza kuwa na mchango mkubwa katika kutatua changamoto zinazoikabili duniani hivi sasa. Nchini Kenya vijana wengi wameitikia wito wa kujumuishwa katika hatua za masuala ya kimataifa ikiwemo vita dhidi ya janga la corona au COVID-19 ambalo linaendelea kuitikisa dunia kwa sasa.