Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya hewa ya Morogoro haikuwa hivi, hatua za pamoja na za haraka zinahitajika-Wakazi wa Morogogo

Hali ya hewa ya Morogoro haikuwa hivi, hatua za pamoja na za haraka zinahitajika-Wakazi wa Morogogo

Pakua

Mkoa wa Morogogoro ulioko katika eneo la mashariki la Tanzania ni moja ya maeneo ambayo kwa miaka mingi yametambulika kuwa maeneo yenye hali nzuri ya hewa kutokana na mazingira yake kuwa yenye misitu, nyika, na milima yenye kutiririsha maji safi. Lakini katika miaka ya hivi karibuni wanaharakati wa kutunza mazingira wanaona kuwa ni muhimu kuchukua hatua za kuilinda hali hiyo kwani iko katika hatari ya kutoweka kutokana na shughuli za binadamu kama vile uchomaji mkaa. John Kabambala wa redio washirika Kids Time FM ya mkoani humo Morogoro, amezungumza na baadhi ya wakazi wa mkoa huo na kutuandalia makala ifuatayo.

Audio Credit
Anold Kayanda\ John Kabambala
Audio Duration
3'36"
Photo Credit
World Bank/Sue Pleming