Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mzee ajikwamua kwa kujiimarisha katika kilimo cha pilipili, Uganda

Mzee ajikwamua kwa kujiimarisha katika kilimo cha pilipili, Uganda

Pakua

Katika juhudu za binafsi za kufikia lengo namba moja la malengo ya maendeleo endelevu au SDGs, mzee mmoja nchini Uganda ameamua kujikwamua kutoka katika lindi la umaskini kwa kujiimarisha katika kilimo cha pilipili.

Mzee Jacob Byemaro wa kijiji cha Bulima tarafa ndogo ya Bwijanga wilayani Masindi, ameamua kurejelea upanzi wa mazao yanayohitaji nguvu kazi kidogo lakini yakitoa mavuno yenye thamani kubwa sokoni.

Je, wajua kwamba nawe pia unaweza kutumia ardhi ndogo na nguvu kazi kidogo ili kujikwamua? Basi sikiliza mahojiano kati ya Mzee huyu na mwandishi wetu wa Uganda, John Kibego.

 

 

 

Attachments area

Audio Credit
Loise Wairimu/John Kibego
Audio Duration
3'40"
Photo Credit
Picha ya IFAD