Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

UN News

Ujumuishwaji ni msingi mkuu katika kusongesha malengo ya maendeleo endevu - Waheshimiwa Baraza na Mugabe

Jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu lijulikanalo kama HLPF linafikia tamati hii leo hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York-Marekani. Wawakilishi wa nchi na serikali, wanasayansi, wanazuoni, mashirika ya umoja wa Mataifa, asasi mbalimbali na vijana wamekutana kuanzia tarehe 10 Julai kujadili hatua za kuchukua ili  kuhakikisha malengo hayo muhimu ya maendeleo yanatimizwa ifikapo mwaka 2030.

Sauti
8'15"
UN/ Anold Kayanda

Vijana wanaweza kutumia elimu yao kusongesha SDGs iwapo watapata ufadhili wa miradi yao - Gibson

Hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa la Umoja wa Mataifa  kuhusu malengo ya maendeleo endelevu  kwa kifupi HLPF linakaribia kufikia ukingoni na leo Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu vijana aliitisha kikao cha kando kuzungumza na vijana kuhusu tathmini yao ya utekelezaji wa Mkakati wa Umoja wa Mataifa kuhusu vijana katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Miongoni mwa walioshiriki ni Gibson Kawago, mmoja wa viongozi vijana wa kusongesha SDGs.

Sauti
2'31"
UN News

Vijana wachukue hatua kuhakikisha malengo ya maendeleo endelevu yanatimizwa - Job Nyangenye Omanga

Jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu lijulikanalo kama HLPF limeingia siku yake ya nne hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York-Marekani. Wawakilishi wa nchi na serikali, wanasayansi, wanazuoni, mashirika ya umoja wa Mataifa, asasi mbalimbali na vijana wanakutana kujadili hatua za kuchukua ili  kuhakikisha malengo hayo muhimu ya maendeleo yanatimizwa ifikapo mwaka 2030. Mmoja wa wanaoshiriki ni Job Nyangenye Omanga, raia wa Kenya anayeishi Texas-Marekani akijishughulisha na sekta ya afya hapa Marekani na nyumbani Kenya.

Sauti
5'14"
UN News

Vijana tusipoteze matumaini bado tuna fursa ya kukabili changamoto ya tabianchi: Omesa Mukaya

Jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu HLPF linaendelea hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambapo wawakilishi wa nchi na serikali, wanasayansi, wanazuoni, mashirika ya umoja wa Mataifa asasi mbalimbali na vijana wanashiriki kukuna vichwa kujadili nini cha kufanyua kuhakikisha malengo hayo muhimu ya maendeleo yanatimizwa ifikpo mwaka 2030 na nini kifanyike kuzisaidia nchi zinazosuasua.

Sauti
6'20"
BAKITA

Mahojiano maalum kuelekea siku ya kimataifa ya lugha ya Kiswahili - BAKITA

Kuelekea siku ya lugha ya Kiswa duniani itakayoadhimishwa Ijumaa wiki hii Afisa habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini Tanzania UNIC Dar es salaam amefunga safari hadi kwenye Baraza la Kiswahili la Taifa nchini humo BAKITA lenye wajibu mkubwa wa kuendelea na kukuza lugha hiyo adhimu sio Tanzania na Afrika tu bali duniani kote  na kuketi chini na mhariri mwandamizi wa Baraza hilo Onni Sigalla. Wamejadili mengi lakini Onni anaanza kufafanua jukumu lake BAKITA.

Sauti
7'16"