Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Alihesabiwa siku za kuishi lakini akaishi zaidi

Umoja wa Mataifa unaendelea kupigia chepuo usambazaji wa huduma za kujikinga na virusi vya ukimwi, VVU ikiwa ni moja ya utekelezaji wa lengo namba 3 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Lengo hilo la ustawi wa afya kwa wote linaangazia siyo tu Malaria na Kifua Kikuu bali pia Ukimwi ambao unaendelea kuwa tishio, licha ya kwamba tayari kuna kinga. Huko nchini Kenya, mwanamke mmoja ambaye baada ya kukatiwa tiketi ya kifo, alikata tamaa akaona dunia imemgeuka. Lakini baada ya kuamua kuchukua hatua, nuru ikaingia na hata akaweza kuongeza familia yake. Je alifanya nini ?

UN Photo/Albert Gonzalez Farran

Kina mama wajasiriamali waneemeka na mafuta Uganda

Upatikanaji wa bidhaa ya mafuta nchini Uganda umeleta faraja kwa mamilioni ya wananchi ambao sasa wanaona nuru ya kupungua kwa bei ya bidhaa hiyo katika siku za usoni. Na neema hiyo sio kwa waendesha magari tu bali pia kwa wafanya biashara ndogondogo au wajasiriamali wakiwemo wanawake. Mwandishi wetu wa Uganda John Kibego amewatembelea baadhi ya wanawake walioanza kunufaika na uwepo wa shughuli za uchimbaji mafuta katika eneo la ziwa Albert nchini humo ili  kupata ufafanuzi zaidi unagana naye

Picha: UNPA

Wasichana Sierra Leone wapingana na wazazi kulinda haki zao

Hebu fikiria mtoto wa kike punde tu baada ya kuzaliwa anafungwa kamba mkononi, ya kwamba ni kishika uchumba kwa kuwa tayari amepata mume. Hiyo inaweza isikuingie akilini iwapo u mkazi wa nchia ambako haki za mtoto zinazingatiwa, hata hivyo nchini Sierra Leone, hilo ni jambo la kawaida na linapatiwa msisitizo kutokana na ukatili wa kijinsia na mila na desturi potofu. Hata hivyo hivi sasa nchini humo wapo watoto wa kike na wasichana ambao wamefunguka macho na wanapingana na hata wazazi wao. Je wanafanya nini?

Sauti
4'12"

Choo chako ni salama?

Utafiti umebaini kwamba ukosefu wa vyoo safi  na salama ni hatarishi kwa afya ya binadamu. Takwimu za mashirika ya ufya ulimwenguni kama WHO na wengine zinaonyesha kuwa jamii zinazoishi katika mazingira yasiyo na vyoo salama zipo katika athari za kupatwa na milipuko ya magonjwa yatokanayo ya ukosefu wa matumizi salama ya vyoo kama kipindupindu na magonjwa mengine.

Dansi ya kitamaduni yaenziwa Uganda

Wakati shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO), linapigia chepuo utunzaji na ukuzaji wa utamaduni,  mjini Hoima nchini Uganda, waimbaji wa kitamaduni waliandaa tamasha la muziki kandoni mwa tamasha za muziki wa kisasa.

Je, lilishindana? Basi ungana na John Kibego katika makala ifuatayo...