Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wasichana Sierra Leone wapingana na wazazi kulinda haki zao

Wasichana Sierra Leone wapingana na wazazi kulinda haki zao

Pakua

Hebu fikiria mtoto wa kike punde tu baada ya kuzaliwa anafungwa kamba mkononi, ya kwamba ni kishika uchumba kwa kuwa tayari amepata mume. Hiyo inaweza isikuingie akilini iwapo u mkazi wa nchia ambako haki za mtoto zinazingatiwa, hata hivyo nchini Sierra Leone, hilo ni jambo la kawaida na linapatiwa msisitizo kutokana na ukatili wa kijinsia na mila na desturi potofu. Hata hivyo hivi sasa nchini humo wapo watoto wa kike na wasichana ambao wamefunguka macho na wanapingana na hata wazazi wao. Je wanafanya nini? Fuatana basi na Joseph Msami kwenye makala hii ikimuangazia msichana shupavu Isha!

Audio Duration
4'12"
Photo Credit
Picha: UNPA