Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Machafuko mapya Sudan Kusini, UNMISS yahifadhi raia zaidi

Machafuko mapya Sudan Kusini, UNMISS yahifadhi raia zaidi

Pakua

Kuzuka kwa machafuko nchini Sudan Kusini mwishoni mwa juma lililopita kumelazimisha vituo vya kuhifadhi wakimbizi wa ndani nchini humo vilivyo chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMSS kujiongeza na kuwahifadhi raia waiso na hatia.

Makala ifuatayo imegubikwa na simulizi za kusikitisha za madhila ya wakimbizi hao ambao sasa mustakabali wao umetatizika. Ungana na Joseph Msami

Photo Credit
Wakimbizi wakiwasili katika sehemu ya hifadhi ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini.(Picha:UNIfeed/video capture)