Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

UN Photo/Sophia Paris

Makala yenye kuangazia siku ya urafiki duniani

Tarehe 30 Julai, jamii ya kimataifa imeadhimisha siku ya urafiki duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akisema urafiki hujenga daraja baina ya watu, na hivyo huchochea amani duniani. Kwenye ujumbe wake kwa siku hiyo, Bwana Ban amesema urafiki ni muhimu sana kwenye dunia ya leo inayokumbwa na ubaguzi, ukatili na mizozo inayoathiri mamilioni ya watu.

UN Photo/Albert Gonzalez Farran

Urafiki wa kweli ni kusaidiana :Waganda

Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Urafiki, inayotumiwa na Umoja wa Mataifa kujenga urafiki na kuunganisha jamii kwa ajili ya amani na ustawi, nchini Uganda raia wa nchi hiyo wanaeleza kwao urafiki una maana gani .

Katika mahojiano na mwandishi wetu John Kibego kutoka Hoima nchini humo, wahojiwa hao wanaeleza mengi lakini kubwa zaidi kwao urafiki ni kusaidiana nyakati zote.

(SAUTI MAHOJIANO)

Mchango wa nyota wa Barcelona kwa watoto

Klabu ya Uhispania ya soka FC Barcelona imo katika ziara ya Amerika Kaskazini, kabla ya msimu mpya wa soka kuanza mnamo mwezi Agosti. Katika hafla moja iliyoandaliwa na Shirika la Kuhudumia Watoto, UNICEF na klabu hiyo ya FC Barcelona, kundi la wanafunzi kutoka mji wa Los Angeles jimboni California, walikutana na nyota wa Barcelona, Andrés Iniesta na Marc-André Ter Stegen kujadili mchango muhimu wa michezo katika maisha ya watoto na maendeleo yao kote duniani.

Kufahamu zaidi yaliyotokea, ungana na Grace Kaneiya katika Makala hii.

Umuhimu wa ujuzi wa vijana katika kujiendeleza

Takriban vijana milioni 74 walikuwa wanasaka ajira mwaka 2014! Hii ni  kulingana na ripoti ya Shirika la kazi duniani ILO. Takwimu za ILO na Shirika la chakula duniani FAO mwaka 2013 zinasema kwamba vijana wanawakilisha asilimia 25% ya wafanyakazi lakini wanajumuisha asilimia 40% ya watu wasiokuwa na ajira.Ili kuimarisha uelewa kuhusu umuhimu wa kuwekeza katika ukuzaji wa ujuzi wa vijana,  Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limeratibu Julai 15 kama siku ya ujuzi wa vijana kimataifa.Siku hii imeadhimishwa kwa mara ya kwanza mwaka huu wa 2015.

Mti Calliandra na manufaa yake

Mti wa Calliandra sasa ni mtaji kwa wakulima, wafugaji na hata katika kutunza mazingira wakati huu ambapo dunia ina kilio cha mabadiliko ya tabia nchi.

Ungana na John Kibego kutoka Uganda kwa makala kuhusu mti huo na manufaa yake kwa makundi hayo na kwa jamii nzima kwa ujumla.

Utunzaji wa mazingira Tanzania wainua kipato

Usafi wa mazingira jijini Mwanza Tanzania sio tu kwamba umewezesha muoneakano bora wa jiji hilo,  bali pia umeinua kipato cha wanavikundi ambao wamelivalia  njuga suala la usafi katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo.

Martin Nyoni wa redio washirika redio SAUT ya Mwanza amezunguka katika maeneo  kadhaa kujionea miradi ya bustani za umwagiliaji na mchango wake katika kutunza mazingira jijini humo.Ungana naye.

Kongamano la tatu la kimataifa kuhusu ufadhili kwa maendeleo-Addis Ababa

Kongamano la tatu la kimataifa kuhusu ufadhili kwa maendeleo limefanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia, kuanzia Jumatatu tarehe 13 hadi Alhamis tarehe kumi na sita wiki hii.

Kongamano hilo liliwaleta pamoja wawakilishi wa kisiasa wa ngazi ya juu, wakiwemo wakuu wa nchi na serikali, mawaziri wa fedha, masuala ya nje na ushrikiano wa maendeleo, wadau wa kitaasisi, mashirika yasiyo ya kiserikali na wanasekta ya biashara.

Elimu ya utambuzi wa fursa kwa vijana inahitajika: Ridhiwani Kikwete

Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya ujuzi kwa vijana inashangaza kuona kuwa baadhi ya vijana wanajishughulisha katika kujikwamua kiuchumi lakini wengi hawafahamu  kuhusu malengo ya maendelo ya milenia amesema mbunge kijana kutoka Tanzania Ridhiwani Kikiwete.

Katika mahojiano na Joseph Msami alipotembelea makao makuu ya Umoja wa Mataifa hivi karibuni, mbunge huyo wa Chalinze mkoani Pwani anasema licha ya fursa lukuki za kimaendeleo ajira ni changamoto kubwa kwa vijana katika  nchi zinazoendelea.

(SAUTI MAHOJIANO)

UN Photo/JC McIlwaine

Uganda yajitutumua katika kukuza elimu ya msingi

Wakati malengo ya maendeleo ya milenia MDGS yakifikia ukomo mwezi Septemba mwaka huu, nchi kadhaa zimejitahidi kutimiza malengo hayo manane likiwemo lengo namba mbili la kukuza elimu ya msingi kwa wote ambapo nchini Uganda serikali kwa kushirikiana na wadau imepiga hatua.

Hatua hizo zimesaidia wanafunzi wengi kujiunga shuleni na hivyo kuanza safari ya kutimiza ndoto zao kama anavyosimulia John Kibego kutoka nchini humo.

Mashirika ya kijamii yataka ahadi za fedha za maendeleo zitekelezwe.

Nchi wanachama za Umoja wa Mataifa zikikutana mjini Addis Ababa nchini Ethiopia kwa ajili ya kongamano la kimataifa kuhusu Ufadhili kwa Maendeleo, mashirika yasiyo ya kiserikali yamekuwa na mkutano maalum mwishoni mwa juma .

Lengo la mkutano huo lilikuwa ni kuunganisha maombi na maoni ya mashirika hayo kuhusu ufadhili kwa maendeleo na kupeleka azimio la pamoja mbele ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Zaidi ya mashirika 400 na wawakilishi 500 wamejisajili kwa ajili ya mkutano huo, wakiwemo wadau kutoka Afrika Mashariki.