Skip to main content

Mashirika ya kijamii yataka ahadi za fedha za maendeleo zitekelezwe.

Mashirika ya kijamii yataka ahadi za fedha za maendeleo zitekelezwe.

Pakua

Nchi wanachama za Umoja wa Mataifa zikikutana mjini Addis Ababa nchini Ethiopia kwa ajili ya kongamano la kimataifa kuhusu Ufadhili kwa Maendeleo, mashirika yasiyo ya kiserikali yamekuwa na mkutano maalum mwishoni mwa juma .

Lengo la mkutano huo lilikuwa ni kuunganisha maombi na maoni ya mashirika hayo kuhusu ufadhili kwa maendeleo na kupeleka azimio la pamoja mbele ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Zaidi ya mashirika 400 na wawakilishi 500 wamejisajili kwa ajili ya mkutano huo, wakiwemo wadau kutoka Afrika Mashariki.

Priscilla Lecomte amekutana nao mjini Addis Ababa. Ungana naye kwenye makala hii.

Photo Credit
Maonyesho ya kabla ya ufunguzi wa Kongamano la FFD3 huko Addis-Ababa Ethiopia.(Picha:Idhaa ya kiswahili/video capture)