Elimu ya utambuzi wa fursa kwa vijana inahitajika: Ridhiwani Kikwete
Pakua
Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya ujuzi kwa vijana inashangaza kuona kuwa baadhi ya vijana wanajishughulisha katika kujikwamua kiuchumi lakini wengi hawafahamu kuhusu malengo ya maendelo ya milenia amesema mbunge kijana kutoka Tanzania Ridhiwani Kikiwete.
Katika mahojiano na Joseph Msami alipotembelea makao makuu ya Umoja wa Mataifa hivi karibuni, mbunge huyo wa Chalinze mkoani Pwani anasema licha ya fursa lukuki za kimaendeleo ajira ni changamoto kubwa kwa vijana katika nchi zinazoendelea.
(SAUTI MAHOJIANO)