Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Waigizaji kutoka Uchina wakumbusha historia ya uhusiano wa biashara

Mwezi huu wa Februari, Uchina ndiyo inayoshikilia kiti cha Urais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Balozi wake Jieyi Liu akiwa na wajibu wa kuongoza vikao vya Baraza hilo.

Kama sehemu ya kusherehekea wajibu huo, Ubalozi wa Uchina umeandaa maonyesho ya ngoma na mchezo wa kuigiza, ambao umekumbusha historia ya uhusiano wa kibiashara karne nyingi zilizopita- biashara ambayo pia ilikuwa sehemu ya kuimarisha uhusiano baina ya mabaharia walioshiriki biashara hiyo, na pia uhusiano baina ya nchi mbali mbali walikotoka mabaharia hao.

UNICEF yahaha kuwanususru wahanga wa mafuriko Malawi

Baada ya kuwa na wakati mgumu kufuatia  mafuriko, wakazi wa Malawi sasa wanapatiwa misaada ya kibinadamu ikiwamo vyombo vy a ndani na malazi.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa kushirikiana na wadau kadhaa wanahakikisha maisha ya watu hawa yanarejea kuwa ya kawaida. Ungana na Joseph Msami katika makala ifuatayo.

Nuru yaangazia askari watoto Sudan Kusini

Nchini Sudan Kusini hatimaye watoto wanaotumikishwa na vikundi vililivyojihami nchini humo sasa wanaanza kuwa na nuru ya matumaini. Hii ni kwa sababu Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto, UNICEF pamoja na wadau wake linahaha kutwa kucha kuhakikisha watoto hao wanaondokana na utumikishwaji huo unaowanyima haki zao za msingi za kuishi, kuendelezwa, kulindwa na kushirikishwa.

Vuta nikuvute baina ya wanyamapori na binadamu Uganda

Uhifadhi wa mazingira ni muhimu katika kuhakikisha uwepo wa wanyamapori na mimea na hata binadamu. Hata hivyo wakati hatua za kudhibiti uharibifu wa mazingira zikiendelea kuchukuliwa, wanyama nao wanatishia uwepo wa binadamu kutokana na vitendo vyao vya kuharibu mazao ambayo ni tegemeo kwa binadamu.

Mathalani nchini Uganda, kuna vuta nikuvute kati ya jamii za wakulima zinazozunguka mbuga za wanyama na wanyama ambao ni kivutio kwa watalii.

Je hali ikoje na hatua gani zinachukuliwa? Basi ungana na John Kibego katika makala ifuatayo.