Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nuru yaangazia askari watoto Sudan Kusini

Nuru yaangazia askari watoto Sudan Kusini

Pakua

Nchini Sudan Kusini hatimaye watoto wanaotumikishwa na vikundi vililivyojihami nchini humo sasa wanaanza kuwa na nuru ya matumaini. Hii ni kwa sababu Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto, UNICEF pamoja na wadau wake linahaha kutwa kucha kuhakikisha watoto hao wanaondokana na utumikishwaji huo unaowanyima haki zao za msingi za kuishi, kuendelezwa, kulindwa na kushirikishwa. Mwaka jana pekee watoto 12,000 walitumikishwa kwenye vikundi hivyo, lakini jitihada za UNICEF sasa zimewezesha watoto hao kuanza kuchiliwa huru na kujumuishwa kwenye jamii kama inavyofafanua makala hii iliyoandaliwa na Assumpta Massoi

Photo Credit
Askari watoto wakati walipokuwa wanakabidhi silaha, magwanda na kukabidhiwa nguo za kiraia. (Picha:Kutoka video ya Unifeed)