Skip to main content

Waigizaji kutoka Uchina wakumbusha historia ya uhusiano wa biashara

Waigizaji kutoka Uchina wakumbusha historia ya uhusiano wa biashara

Pakua

Mwezi huu wa Februari, Uchina ndiyo inayoshikilia kiti cha Urais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Balozi wake Jieyi Liu akiwa na wajibu wa kuongoza vikao vya Baraza hilo.

Kama sehemu ya kusherehekea wajibu huo, Ubalozi wa Uchina umeandaa maonyesho ya ngoma na mchezo wa kuigiza, ambao umekumbusha historia ya uhusiano wa kibiashara karne nyingi zilizopita- biashara ambayo pia ilikuwa sehemu ya kuimarisha uhusiano baina ya mabaharia walioshiriki biashara hiyo, na pia uhusiano baina ya nchi mbali mbali walikotoka mabaharia hao.

Mwenzetu Joshua Mmali alikuwa miongoni mwa watazamaji, na katika makala hii, anatupeleka kwenye ukumbi wa Baraza Kuu kutumegea kidogo yaliyokuwemo.

Photo Credit
Dansi wakati wa hafla iliyofanyika hapa makao makuu(Picha ya UM/Loey Felipe)