Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Safari bado ni ndefu kufikia elimu bora kwa wote

Safari bado ni ndefu kufikia elimu bora kwa wote

Pakua

Katika baadhi ya maeneo ya Kenya, Argentina, India au Morocco, watoto bado wanahangaika kufika shuleni kila siku. Filamu ya kifaransa "Sur le Chemin de l'école", yaani wakati wa kwenda shuleni, inaonyesha maisha ya watoto hao. Jackson, ambaye anaishi kaskazini mwa Kenya, anakimbia zaidi ya kilomita 15 ili afike shuleni kila siku, akikutana wanyamapori njiani.Priscilla Lecomte ameongea na mtengenezaji wa filamu Pascal Plisson pamoja na Naibu mwakilishi wa kudumu wa Kenya katika Umoja wa Mataifa, Koki Muli Grignon, ambao wamehudhuria maonyesho ya filamu hii katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa, hivi karibuni. Ungana nao katika makala hii!

Photo Credit
Jackson na mdogo wake Salome wakikimbia kwenda shuleni, nchini Kenya. Picha Distrib Films US.