Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Uhaba wa vyoo wahatarisha afya za wananchi nchini Kenya

Dunia ikiadhimisha siku ya choo duniani leo Nov 19, 2013 baadhi ya nyumba bado hazina vyoo. Takwimu zinaonyesha kuwa watu zaidi ya bilioni 2.5 kote duniani hawana vyoo hatua inayoweza kusababisha matatizo ya afya kwao. Mwandishi wetu Jasson Nyakundi anamulika hali ilivyo nchini Kenya ambapo anazungumza na Samwel Waweru akiwa Mukuru Kwa njenga anayemiliki choo cha biashara.

Huu ni ushindi kwa Afrika, haturudi nyuma -Balozi Macharia

Mwakilishi wa kudumu wa Kenya kwenye Umoja wa Mataifa balozi Macharia Kamau amesema kile kinachoonekana kama kushindwa kwa ombi la Umoja wa Afrika kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa la kutaka kusitishwa kwa uchunguzi na mashtaka dhidi ya viongozi wa Kenya yaliyoko Mahakama ya kimataifa ya Uhalifu, ICC ni ushindi mkubwa kwa Afrika.

Ugonjwa wa Kisukari umebadili maisha yangu: Mkazi wa Tanga, Tanzania

Mtu anapopatiwa taarifa ya kwamba ana ugonjwa wa Kisukari, punde maisha yake hubadilika! Hulazimika kuchukua hatua kadhaa ikiwemo matibabu ya kila siku, kubadili mlo na hata mfumo wa maisha. Kama mtu alizowea mtindo fulani wa maisha hulazimika kubadili iwapo anataka kupata ahueni au kudhibiti ugonjwa huo. Shirika la afya duniani linasema hivi sasa kuna wagonjwa Milioni 350 duniani kote, na idadi itaongezeka kwa kuwa mazingira yaliyopo ni stahili kwa hilo. Mathalani vyakula vyenye mafuta mengi, watu kutokufanya mazoezi na unywaji wa vileo.

Mchezo wa baiskeli ni mtaji wa mshikamano Rwanda

Rwanda, taifa ambalo lilitatizika kwa mauaji ya halaiki takribani miaka 20 iliyopita, sasa liko katika mchakato wa utangamano. Hatua hii jumuishi inahitaji sekta zote kuwajibika, na hii ndio sababu ya kuanzisha mchezo wa basikeli wenye lengo la kuwaweka vijana  na kamundi mbalimbali pamoja bila kujali tofauti zao.

 Ungana na Joseph msami katika makala inayomulika filamu iitwayo Amka majivuni ambayo kwayo utafahamu jinsi mchezo wa baiskeli ulivyotumika kuhamasisha umoja na mashikamano nchini humo.

Makosa kwenye mikataba ya awali kuhusu mabadiliko ya tabianchi kuepukwa: Dokta Muyungi

Wataalamu wa masuala ya mabadiliko ya tabianchi wanaendelea na kikao chao huko Warsaw Poland, matarajio ni kufikiwa makubaliano mapya ifikapo mwaka 2015 kuhusu hali ya hewa kwa mustakhbali endelevu wa dunia, wakati huu ambapo madhara yatokanayo na mabadiliko hayo hayachagui nchi maskini wala tajiri. Dokta Richard Muyungi, ni Mwenyekiti wa Kamati ya dunia ya Kisayansi na Taaluma ya mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi na akiwa Warsaw alizungumza kwa njia ya simu na Assumpta Massoi wa Idhaa hii kuhusu majaliwa ya kikao hicho ikiwemo mbadala wa biashara ya hewa ya ukaa.

Maji utapiamlo vyapata suluhu Ethiopia

Maji yamekuwa ni kitendawili ambacho hakina jibu nchiniEthiopiakwa muda mrefu hususani maeneo ya vijijini. Huduma ya lishe nayo si shwari. Katika jamii yenye changamotokamahizo maisha huwa kizungumkuti. Lakini waswahili alisema nyota njema huonekana asubuhi, na hiki ndicho kilichotokea hukoEthiopia.

Kufahamu undani wa hatma ya huduma hizi, ungana na Joseph Msami katika makala ifuatayo.

Usimamizi mzuri unakwenda sambamba na uhamiaji mzuri

Maafisa wa uhamiaji wa kutoka Sudan Kusini walisafiri hadi Tanzani kushiriki katika mafunzo yaliotolewa na Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM . Mafunzo hayo yalilenga kuwafunza kuhusu njia bora za kudhibiti mipaka na pia kuwakutanisha na maafisa wa uhamiaji wa Tanzania. Assumpta Massoi wa Idhaa hii aliongea na msemaji wa IOM Jumbe Omari Jumbe ambaye anaanza kwa kueleza IOM  lilivyowezesha mafunzo hayo.

(MAHOJIANO)

UNICEF yapigia chapuo afya ya mama na mtoto India

Shirika la umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa kushirikiana na serikalai ya India linasaidia kuinua sekta ya afya nchini humo hususani kwa kina mama na watoto. UNICEF imewekeza katika raslimali watu na vifaa  na kuleta mabadiliko makubwa.

Joseph Msami anafafanua vyema katika makal ifuatayo.