Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahojiano

Tunajali haki za walemavu: Tanzania

Haki na ustawi wa watu wenye ulemavu ni kipaumbele cha serikali ya Tanzania, amesema rais wa nchi hiyo Jakaya Kikwete wakati akihutubia taifa hilo kwenye maadhimisho ya siku hiyo yaliyofanyika kitaifa mjini Dar es salaam.

Wakati rais Kikwete akisisitiza kujali maslahi ya kundi hilo, walemavu wenyewe wanadai bado hawapati msaada kama wanavyotarajia. Mwandishi wa radio washirika Wapo Fm ya jijini Dar es salaama Anthon Joseph ameandaa taarifa ifuatayo.

Tamasha la uelewa wa Ukimwi lafanyika Tanga, Tanzania

 

Wakati dunia ikiadhimisha siku ya ukimwi duniani mwishoni mwa wiki, maadhimisho haya yameleta mwanga bora mkoani Tanga nchini Tanzania ambapo tamasha kubwa limefanyika katika wailaya ya Pangani ili kukuza uelewa wa wananchi.

Muhamedi Hamie kutoka radio washirika Pangani Fm, Tanga Tanzania, amefika katika tamasha hilo na kuandaa makala ifuatayo

Upatikanaji wa maji ni habari njema kwa jamii ya wafugaji Tanzania

Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wahisani imekuwa ikijitahidi kutekeleza malengo ya maendeleo ya milenia katika maeneo mbalimbali ikiwamo kuboresha huduma ya maji vijijini na mijini.

Makala ifuatayo inaangazia miongoni mwa eneo kame kabisa Kaskazini mwa nchi hiyo ambapo kwa asilimia kubwa jamii ya wafugaji wa kimasaia ndiyo inaishi huko. Ungana na Joseph Msami.

Hali ya usalama bado ni tete CAR; Mia Farrow ashuhudia

Huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, hali ya usalama inazorota lakini juhudi za Umoja wa Mataifa zinaendelea ili kusaidia waathirika wa mgogoro unaondelea nchini humo.

Juhudi za hivi karibuni zaidi ni ziara ya balozi mwema wa shirika la Umoja UNICEF Mia Farrow aliyefika CAR kuanagalia athari za mgogoro. Ungana Na Joseph Msami katika makala inayongazia ziara yake.

Masaibu ya wakimbizi wa Syria walioko Lebanon yaangaziwa

Siku chache baada ya Umoja wa Mataifa kutangaza tarehe 22 January mwakani ya kufanyika kwa mkutano wa pili wa amani kuhusu Syria huko Geneva, wakimbizi wa nchi hiyo walioko katika kambi nchini Lebanon wanaelezea madhila wanayokutana nayo.

Hapa katika mji wa Arsal nchiniLebanonkuna foleni kubwa ya watu nje ya kituo cha usajili. Zaidi ya familia 60 wamepata makazi katika msikiti akiwamo Muhamed kutokaHomshuku wengine wakiwa katika  chumba cha harusi aliyefika hapa siku mbili zilizopita na mke wake na mtoto. Familia hii imehama karibu mara tano sasa tangu mzozo huu ulipoanza.

Athari ya taka ya mafuta yaangaziwa Uganda

Serikali ya Uganda ilitangaza ugunduzi wa mapipa bilioni 3.5 ya mafuta chini ya bonde la ufa la Ziwa Albert . Utafutaji wa mafuta unaendelea wakati moja na mandalizi ya kwanza kuyazalisha.

Wanamazingira wanaonya kuwa uvuvi utaathiriwa kwa sababu wanaona serikali haijajiandaa kukabiliana na athari za mafuta kwa mazingira.

(MAKALA YA JOHN KIBEGO RADIO WASHIRIKA SPICE FM, UGANDA)

Ukatili wa kingono wapigwa vita nchini Kenya

Wakati dunia ikiadhimisha mkataba wa watoto unaolinda haki za kundi hilo muhimu katika jamii, nchini Kenya, kama kwingineko duniani, visa vya ubakaji vinatajwa. Hata hivyo katikati ya wingu hilo la ukatili wa kingono kuna habari njema za kuwanusuru wahanga wa matuko hayo.

Ungana na Joseph Msami katika makala ifuatayo .

IOM yawakwamua wahamiaji wasio na nyaraka toka Tanzania walio mipakani huko Maziwa makuu

Taarifa zinasema maelfu ya wahamiaji kutoka Tanzania wamekwama mipakani huku hali ya wasiwasi juu ya majaliwa yao ikiibuka. Hii inafuatia zoezi la serikali ya Tanzania kuwaondoa wahamiaji hao katika zoezi lililotangazwa na kutekelezwa na serikali hiyo. Hivi karibuni.

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limejikita kuwasaidia wakimbizi hao kama msemaji wa shirika la uhamiaji IOM Jumbe Omari Jumbe aanavyofafanua alipohojiwa na Joseph Msami wa idhaa hii.

(MAHOJIANO)

Mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi, maafikiano yacheleweshwa na malumbano

Wakati kikao cha kumi na tisa cha mkutano wa mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabia kikielekea mwisho taarifa zinasema hali ni tete katika mijadala ambapo mabishano yameibuka kati ya nchi zinazoendelea na zile zilizoendelea . Malumbano hayo yamesababisha vikao kufanyika hadi usiku wa manane na wakati mwingine baadhi ya wawakilishi kutoka nje kama ishara ya kutokubaliana na mapendekezo au  hoja.