Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

15 Juni 2022

Jaridani Jumatano, Juni 15, 2022 na Leah Mushi

-Shida na changamoto nyingi zinazowakumba wanawake ni kutokana na mfumo dume na uchu wa madaraka: Guterres

-Mtoto asimulia safari ya Bunagana hadi Rutshuru nchini DRC

-Makala inamulika changamoto na jitihada za kufikia lengo la huduma za afya kwa wote nchini Tanzania kabla ya ukomo wa malengo ya maendeleo endelevu SDGs.

-mashinani tutaelekea katika Wilaya ya Kaabong, Mkoa wa Karamoja nchini Uganda kumsikiliza kijana aliyekuwa mchunga ng’ombe na sasa ameianza safari ya kuisaka elimu

Sauti
11'53"

14 Juni 2022

Jaridani Jumanne Juni 14-2022 na Leah Mushi

-Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani, WFP limesema limelazimika kusitisha mgao wa chakula Sudan Kusini kutokana na ukata, hali ambayo itaacha theluthi moja ya wakazi wa taifa hilo changa zaidi duniani bila uhakika wa chakula na wengine milioni 1.7 hatarini kufa kwa njaa. 

13 Juni 2022

Jaridani Jumatatu, Juni 13-2022 na Leah Mushi

-Ikiwa leo dunia inaadhimisha siku ya kimataifa ya kuelimisha jamii kuhusu watu wenye ualbino, Umoja wa Mataifa umetoa rai kwa nchi zote duniani kuwajumuisha watu wenye ualbino katika mijadala na mipango inayoathiri haki zao za kibinadamu, ili kuhakikisha wanafurahia usawa na ulinzi unaotolewa kwao katika sheria na viwango vya kimataifa.

Sauti
12'24"

10 Juni 2022

Jaridani Ijumaa, Juni 10-2022 na Leah Mushi-

-Sekta zote zihusishwe ili kuondoa tatizo la ajira za watoto Guatemala

-Ili kuhakikisha uhakika wa chakula duniani, IFAD yawekeza kwenye soko la hisa

Kwenye makala tupo Tanzania katika mkoa wa Morogoro ambako kwa usimamizi wa serikali ya nchi hiyo kwa kushirikiana na wadau wao, kumezinduliwa programu jumuishi ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto kwa lengo la kuchangia katika kumaliza changamoto ya lishe duni na ukatili kwa watoto walio chini ya umri wa miaka nane.

Sauti
9'59"

09 Juni 2022

Jaridani Alhamisi Juni 9,2022 na Leah Mushi-

-Ripoti mpya ya mtazamo wa chakula duniani iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO inasema watu wasiojiweza na walio hatarini duniani ndio wanaolipa gharama kubwa kwa chakula kidogo na hivyo kuwaweka katika hatari kubwa ya kutokuwa na uhakika wa chakula kutokana na bei za juu za chakula hicho na pembejeo za kilimo.

Sauti
12'42"

08 Juni 2022

Jaridani Jumatano Juni 8-2022 na Leah Mushi

-Ikiwa leo ni siku ya bahari duniani, Umoja wa Mataifa unapazia sauti umuhimu wa kulinda bahari ambayo ni chanzo cha zaidi ya asilimia 50 ya hewa ya Oksijeni inayotumika duniani.

-Shirika la Umoja wa Mataifa lakuhudumia watoto UNICEF limesema hali ni tete na watoto zaidi ya laki 3 na themanini wana utapiamlo mkali nchini Somalia ambapo hata ukiwaona watoto hao machozi yatakutoka.

Sauti
9'58"

07 Juni 2022

Leo jaridani ni mada kwa kina ambapo tunakwenda huko Kenya ambako katika eneo la Turkana, Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na serikali mradi wa visima vinavyotumia nishati ya jua katika baadhi ya maeneo ya Turkana ambako wanadamu na wanyama awali walikuwa wanayemelewa na kifo kutokana na ukame. Lakini kwanza ni habari kwa ufupi zikimulika:

Sauti
11'34"

06 Juni 2022

Hii leo jaridani Leah Mushi anaanzia nchini Rwanda kunakofanyika mkutano wa kimataifa kuhusu mawasiliano na kisha anakupeleka Kenya kusikia maoni kuhusu  umuhimu wa bahari katika maisha ya Bernadatte Loloju asemaye kuwa "Bahari ni uhai, sio kwangu mimi tu bali kwa Wakenya wote." Makala inamulika usalama wa chakula kuelekea siku ya usalama wa chakula duniani kesho Juni 7 na tunakwenda Tanzania. Mashinani tunammulika mwananchi wa Kenya ambaye mabadiliko ya tabianchi yamemlazimu kuacha ufugaji na kugeukia uvuvi. Karibu!

Sauti
9'59"

3 Juni 2022

Jaridani Juni 3, 2022 na Leah Mushi

-Siku 100 za uvamizi wa Urusi kwa Ukraine, ustawi wa watu umeathirika sana

-Nchi zatakiwa kuimarisha huduma za afya ya akili wakati zikikabiliana na mabadiliko ya tabianchi

-Katika makala tunaelekea kaunti ya Nyeri kwa vijana wakulima

-Mashinani tutasikia kuhusu ugonjwa wa Monkey Pox na wito wa kukabiliana na magonjwa ya milipuko kwa pamoja

Sauti
12'8"