Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

13 Juni 2022

13 Juni 2022

Pakua

Jaridani Jumatatu, Juni 13-2022 na Leah Mushi

-Ikiwa leo dunia inaadhimisha siku ya kimataifa ya kuelimisha jamii kuhusu watu wenye ualbino, Umoja wa Mataifa umetoa rai kwa nchi zote duniani kuwajumuisha watu wenye ualbino katika mijadala na mipango inayoathiri haki zao za kibinadamu, ili kuhakikisha wanafurahia usawa na ulinzi unaotolewa kwao katika sheria na viwango vya kimataifa.

-Tuzo ya kila mwaka ya shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi, UNFPA ambayo hutolewa kwa mtu binafsi na shirika au taasisi inayojikita katika kuboresha afya ya uzazi kwa wanawake, pamoja na afya ya akina mama na wajawazito, mwaka huu imeenda kwa Emma Theofelus ambaye ni Naibu Waziri wa Habari wa sasa nchini Namibia na mshindi wa kwanza mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kupata tuzo hiyo.

-Kwenye makala ni kuhu sera inayosimamia sekta za kilimo, uvuvi na mifugo nchini Tanzania na hatua gani zichukuliwe kukabili madhara ya tabianchi kwa sekta hizo.

-Katika mashinani tupo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kushuhudia ndege zisizo na rubani au Drones katika utoaji afya.

 

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
12'24"