Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

08 Juni 2022

08 Juni 2022

Pakua

Jaridani Jumatano Juni 8-2022 na Leah Mushi

-Ikiwa leo ni siku ya bahari duniani, Umoja wa Mataifa unapazia sauti umuhimu wa kulinda bahari ambayo ni chanzo cha zaidi ya asilimia 50 ya hewa ya Oksijeni inayotumika duniani.

-Shirika la Umoja wa Mataifa lakuhudumia watoto UNICEF limesema hali ni tete na watoto zaidi ya laki 3 na themanini wana utapiamlo mkali nchini Somalia ambapo hata ukiwaona watoto hao machozi yatakutoka.

Katika makala tunakwenda Vanga Pwani ya Kenya kwenye mpaka na Tanzania katika Bahari ya Hindi kuzungumza na wananchi kuhusu kulinda mazingira ya bahari.

Mashinani ni ujumbe wa umuhimu wa kulinda mazingira ya bahari.

 

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
9'58"