Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

11 Mei 2021

Ghasia zaendelea Yerusalem Mashariki, UN yapaza sauti. 

Juhudi za kujikwamua na COVID-19 zakumbana na kigingi, huku gonjwa wakiongezeka, imesema ripoti ya hali na matarahjio ya uchumi duniani, WESP.

Na ufadhili wa Benki ya dunia kwa nishati ya jua, nuru kwa wafanyabiashara Somalia.

Sauti
12'48"

10 Mei 2021

Kupitia mada kwa kina ya Jarida la Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, Leah Mushi anachambua faida za ndege wahamao, ambao huadhimishwa kila Jumamosi ya tarehe 8 Mei ikiwa ni njia mojawapo ya kutambua faida zao katika maisha ya binadamu na sayari dunia. 

Sauti
11'41"

07 Mei 2021

Katika mada kwa kina, vijana nchini Tanzania wamechukua hatamu ya maisha yao kwa kujiunga katika umoja ili kutekeleza azma ya Umoja wa Mataifa ya kuondokana na umaskini ifikapo mwaka 2030. Mwenyeji wetu katika mada kwa kina in Leah Mushi!Karibu!

Sauti
11'10"

06 Mei 2021

ICC yamfunga jela kamanda wa waasi nchini Uganda.

Ulemavu sio kulemaa - Fahad na Ester wa Geita, Tanzania.

Na mkimbizi Muhammad toka Eritrea aeleza namna UNHCR imerejeshea matumaini ya maisha. 

Sauti
15'5"

05 Mei 2021

Kufuata takwimu na kuwekeza kwa wakunga ni jibu la uhai wa mama na mtoto, inasema UNFPA katika kuadhimisha siku ya wakunga duniani.

Viwango vipya vya WHO kuzisaidia nchi kupunguza ulaji wa chumvi na kuokoa maisha.

Nchi yako ni kama mama na kujitenga nayo ni mtihani, anasema Mkimbizi Donatien wa Burundi aliyeishi Rwanda kwa muda wa miaka 4 na sasa amerejea nyumbani na familia yake kupitia mpango wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.

Sauti
12'38"

04 Mei 2021

COVID-19 imeigharimu India kwa kutozingatia masharti na kuchukua hatua mapema, imeeleza WHO.

Nimesomea umeme, nawazaje kuwa mfugaji wa kuku?

Na kuelekea siku ya wakunga duniani, Chama cha wakunga Tanzania, wapanga kuongelea umuhimu wa kuwekeza kwa mkunga. 

Sauti
11'51"

03 MEI 2021

 Ahimidiwe Olotu wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa, UNIC jiijni Dar es salaam, chini Tanzania kumulika warsha iliyofanyika kuelekea sku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani ambayo imeadhimishwa hii leo kote duniani. 

Sauti
12'21"