Kamishna Mkuu wa UNHCR akiwa ziarani Ethiopia anasihi wasisahaulike wanaoikimbia Sudan
Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Filippo Grandi akihitimisha ziara ya siku tatu nchini Ethiopia ametoa wito kwa ulimwengu kuwasaidia watu wa Sudan wanaoikimbia nchi yao na kuingia Ethiopia ambayo ni moja ya nchi wenyeji wa wakimbizi na wakimbizi wa ndani wengi zaidi ulimwenguni.
“Kuna majanga mengine kote duniani. Mengine makali zaidi na mengine yanaongelewa zaidi. Tusiwasahau watu ambao nimezungumza nao waliokimbia vita Sudan. Hawa wanateseka kila siku na wanahitaji msaada.”