Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi 5 zapokea vyeti kutoka WHO kwa kuchukua hatua kutokomeza vambato hatari kwenye vyakula

Nchi 5 zapokea vyeti kutoka WHO kwa kuchukua hatua kutokomeza vambato hatari kwenye vyakula

Pakua

Kwa mara ya kwanza leo shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani, WHO, limezitunukia vyeti nchi tano kwa hatua kubwa zilizopiga katika kutokomeza viambato vya mafuta katika vyakula vinavyosindikwa viwandani kwa ajili ya kuongeza ladha au Trans Fats. Flora Nducha na maelezo zaidi.

Kwa nmujibu wa WHO nchi hizo tano zilizopokea vyeti leo mjini Geneva Uswisi ni Denmark, Lithuania, Poland, Saudi Arabia na Thailand na zimepongezwa kwa kuwa na será bora kwa ajili ya kutokomeza viambato hivyo vya mafuta kwa vyuakula vinavyosindikwa viwandani au iTFA na pia mfumo wa kufuatilia utekelezaji wa serra hizo.

Ingawa lengo la WHO lililowekwa mwaka 2018 la kutokomeza viambato vya mafuta y kuongeza ladha katika vyakula vinavyosindikwa viwandani ifikapo mwisho wa mwaka 2023 halikutimia shirika hilo linasema kuna hatua kubwa zimepigwa kuelekea utimizaji wa lengo hilo katika kila kanda duniani.

Mathalani limesema mwaka jana pekee nchi saba ziliweka na kuanza kutekeleza será za kutokomeza viambato hivyo vya mafuta ambazo ni Misri, Mexico, Moldova, Nigeria, North Macedonia, Ufilipino na Ukraine.

Viambato vya mafuta katika chakula vinahusishwa na athari nyingi za kiafya zikiwa ni pamoja na ongezeko la magonjwa ya kiharusi, shinikizo la damu na vifo vitokanavyo na magonjwa ya moyo.

Baadhi ya vyakula vyenye kiwango kikubwa cha viambato hivyo vya mafuta WHO inasema ni vuakula vya kukaangwa, keki na miliambayo imeshatayarishwa na kufungashwa viwandani ambavyo vina viwango vya juu vya sukati, mafuta na chumvi.

Akikabidhi vyeti hivyo mkuruhenzi mkuu wa WHO Dkt. Tedros Adhanon Ghebreyesus amesema “ Viambato vya mafuta havina faida yoyote mwilini isipokuwa hatari kubwa. Tunafuraha kwamba kuna nchi nyingi zimeweka será za kutokomeza au kupunguza viambato vya mafuta katika chakula. Lakini kuweka será ni suala moja na kuzitekeleza ni suala lingine. Nazipongeza Denmark, Lithuania, Poland, Saudi Arabia na Thailand kwa kuingoza Dunia katika kufuatilia na kutekeleza será dhidi ya viambato vya mafuta katika chakula, tunazichagiza nchi zingine kufuata nyayo zao.”

Hivi sasa shirika hilo linasema kuna jumla ya nchi 53 zimeweka será na kuanza kuzitekeleza dhidi ya viambato vya mafuta katika chakula na hivyo kuboresha lishe ya watu bilioni 3.7 sawa na asilimia 46 ya watu wote duniani ikilinganishwa na asilimia 6 tu ya watu miaka mitano iliyopita.

 

 

 
Audio Credit
Anold Kayanda/Flora Nducha
Audio Duration
2'38"
Photo Credit
Public domain