Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali si swari Burkina Faso msirejeshe wakimbizi wake: UNHCR

Hali si swari Burkina Faso msirejeshe wakimbizi wake: UNHCR

Pakua

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR, leo limetoa mwongozo mpya juu ya ulinzi wa watu wanaokimbia Burkina Faso, na wito wa haraka kwa mataifa yote kuacha kuwarudisha kwa nguvu watu wote wanaotoka katika ukanda huo ulioathiriwa zaidi na mgogoro unaoendelea nchini humo na badala yake kuwaruhusu raia wanaokimbia Burkina Faso kuingia katika mipaka yao. 

Huku hali ya usalama nchini Burkina Faso ikiendelea kuzorota, UNHCR imesema ina wasiwasi mkubwa kutokana na kuenea kwa hali ya ukosefu wa usalama na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa dhidi ya raia.

Ukwiukwaji huo ni pamoja na mauaji, kutoweshwa kwa lazima, mateso na utekaji nyara. 

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva uswis hii leo Elizabeth Tan, mkurugenzi wa ulinzi wa kimataifa wa UNHCR amesema: “Katika matukio kadhaa, raia wamekuwa wakilengwa na kuuawa, na hivyo kusababisha vifo vingi vya raia na watu kutawanywa. Watoto pia wanakabiliwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, kama vile kuajiriwa kwa nguvu vitani na makundi yenye silaha, ajira ya watoto, pamoja na aina nyingine za unyanyasaji, ukatili, unyonyaji na unyanyasaji wa kijinsia."

Ameongeza kuwa asilimia kubwa ya watu wanaotawanywa ni watoto, shule nyingi zimelazimika kufungwa na takriban asilimia 82 ya wasichana wanakabiliwa na ukatili wa kijinsia, lakini pia mamilioni wanahitaji msaada.

Anasema "Takriban watu milioni 4.7 kote nchini wanahitaji msaada wa kibinadamu, na ikiwa ni zaidi ya asilimia 20 ya wakazi wote wa nchi hiyo."

Kwa mujibu wa UNHCR vita na machafuko pia vimesambaratisha mioundombinu na kuathiri huduma za serikali na taasisi ikiwemo katika maeneo yaliyoathirika na vita na hali ni mbayá zaidi kwa watu wanaoishi katika miji ambayo makundi yenye itikadi Kali yanazuia watu ikiwemo idadi kubwa ya wakimbizi wa ndani.

Hadi kufikia Juni mwaka huu wa 2023, zaidi ya watu 67,000 kutoka Burkina Faso wamesaka hifadhi katika nchi jirani kama vile Mali, Niger, Ivory Coast, Togo, Benin na Ghana, huku zaidi ya watu milioni 2 wakiwa wakimbizi wa ndani katika nchi yao, na kuufanya mzozo huo kuwa moja ya mizozo mibaya zaidi yawakimbizi wa ndani katika bara la Afrika.

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
2'33"
Photo Credit
© UNHCR/Insa Wawa Diatta