Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Upandaji wa miti ya migunga yarejesha matumaini kwa wakazi wa msitu wa Congo

Upandaji wa miti ya migunga yarejesha matumaini kwa wakazi wa msitu wa Congo

Pakua

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, mradi unaofadhiliwa na Benki ya Dunia wa kupanda miti aina ya migunga umeondoa tishio la ukataji miti holela kwenye msitu.

wa bonde la mto Congo, ambao ni wa pili kwa ukubwa duniani katika kufyonza hewa ya ukaa na sasa wananchi wananufaika sio tu kwa kupata mkaa bali pia hata watu wa jamii ya asili wanaweza kupata kitoweo porini.

Video ya Benki ya Dunia inaanzia kwenye msitu wa bonde la Mto Congo ambako yaelezwa ekari nusu milioni ya misitu ya asili hutoweka kila mwaka kutokana na ukataji miti kwa ajili ya shughuli za kilimo, kuni na kuchoma mkaa.

Tunalima ardhi na kila siku nakata matawi ya miti na kuchanja ndoo moja ya kuni,” anasema Nzaka Ilanga akiwa porini akikata kuni akiendelea kusema zikiisha kesho tena narudi nakata nyingine kupikia chakula kwa ajili ya watoto.”

Kwingineko anaoneka Guysha Izemengwe akichoma mkaa akisema anatumia miti midogo midogo kuchoma mkaa akisema anapata magunia 22 ya mkaa na kila moja anauza faranga 7,000 za DRC sawa na dola 3 na senti 50 na hiyo ndio chanzo cha kipato kwa familia yake.

Kwa mujibu wa Benki ya Dunia ni asilimia 3.7 tu ya wananchi wa DRC ndio wanapata nishati ya kisasa ya kupikia.

Shinikizo la ukataji miti holela linaweka mashakani wale wanaotegemea zaidi kwa chakula kama vile watu wa asili jimboni Mai- Ndombe ambapo Deko Louis akiwa anatembea msituni anasema…mitego yangu iko porini. Nawinda wanyama kwa ajili ya familia yangu. Siku hizi ni vigumu sana kupata

wanyama. Si unaona leo nzima hatujapata mnyama. Zamani tungalikuwa tumepata hata Kobe.”

Benki ya Dunia ikaja na mradi wa kupanda misitu mipya kwa kutumia miti ya migunga. Wakulima awali walikuwa na wasiwasi lakini sasa ndani ya misitu hiyo wamepanda na mihogo.

Mayasa Mpime mkulima huyu akiwa kwenye msitu huo wa kupanda anasema uyoga ambao awali ilikuwa vigumu kupata sasa inachipuka tena. Na hata tunaweza kuwinda swala ndani ya msitu huu. Hivyo tunakula vizuri. Pia tunarina asali ambayo tunatumia na pia tunauza.”

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
2'16"
Photo Credit
World Bank video