Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakati wa COVID-19 watoto milioni 25 walikosa chanjo, ni wakati wa kuziba pengo hilo: WHO

Wakati wa COVID-19 watoto milioni 25 walikosa chanjo, ni wakati wa kuziba pengo hilo: WHO

Pakua

Wiki ya chanjo ya shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani WHO, inaanza leo ikichagiza juhudi kubwa kufanyika ili kuziba pengo la chanjo duniani kote.

Wiki hiyo itakayo kamilika Aprili 30 huadhinmishwa kila wiki ya mwisho ya mwezi Aprili lengo likiwa ni kuainisha juhudi za pamoja zinazohitajika ili kuwalinda watu dhidi ya magonjwa yanayozuilika kwa chanjo.

Katika wiki hii ambayo imebeba kaulimbiu “The Big Catch-Up” ikisisitiza juhudi kubwa zinazohitajika katika kibarua kilichopo kufikia lengo la chanjo, WHO inashirikiana na wadau mbalimbali kuzisaidia nchi kurejea katika msitari unaotakiwa kuhusu chanjo ili kuhakikisha watu wengi zaidi wanalindwa dhidi ya magonjwa yanayozuilika.

WHO inasisitiza kwamba “Tunahitaji kuchukua hatua sasa ili ili kuwafikia mamilioni ya Watoto ambao walikosa chanjo wakati wa janga la coronavirus">COVID-19, kurejesha usambazaji wa chanjo muhimu kwa kiwango cha angalau mwaka 2019 na kuimarisha huduma za msingi za afya ili kuweza kutoa chanjo.”

Kwa mujibu wa shirika hilo la afya duniani lengo kubwa la wiki ya chanjo duniani ni kwa watoto wengi, watu wazima na jamii zao kulindwa dhidi ya magonjwa yanayozuilika kwa chanjo kama polio, surua, pepopunda na mengine na kuwaruhusu kuishi kwa furaha na kuwa na maisha yenye afya.

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
2'34"
Photo Credit
© UNICEF/Kalungi Kabuye