Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkulima wa maharage nchini Rwanda aeleza mafanikio anayopata

Mkulima wa maharage nchini Rwanda aeleza mafanikio anayopata

Pakua

Kutana na mkulima Immaculée kutoka Rwanda ambaye anajivunia sio tu kupata kipato kujikimu kimaisha kutokana na mahindi na maharage anayolima bali pia jinsi mazao yake yanavyosaidia kuwa neema kwa mamia ya watoto kupitia mlo shuleni. Flora Nducha anasimulia zaidi 

(TAARIFA YA FLORA NDUCHA) 

Immaculée mkulima mdogo wa maharage na mahindi nchini Rwanda akisema anahisi Faraja kubwa kutambua kwamba mazao ya jasho lake yanawafilia mamia ya Watoto katika program ya shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP ya kuwapatia mlo Watoto mashuleni ikiwemo katika jamii yake. 

“Kinachonihamasisha zaidi ni kujua kwamba WFP inanunua nincahozalisha na kusambaza mashuleni ambako watoto kutoka katika jamii yetu wanapata mlo shuleni” 

Kama mkulima mdogo aliyejikita na kilimo cha maharage yenye madini chuma kwa wingi anakabiliwa changamoto lukuki lakini mwaka 2018 chama cha ushirika anachokiuzia mazao yake kikaanza kupata msaada kutoka WFP hasa kwa kununua maharage hayo kwa ajili ya program yake ya mlo shuleni nchini Rwanda ambayo lengo lake kuwa ni kuhakikisha Watoto wanapata lishe na kuendelea kusoma lakini pia wakulima wanaozalisha lishe hiyo wanafaidika kiuchumi 

“Inachokifanya WFP ni kuunganisha chama chetu cha ushirika na masoko kwa mfano katika msimu uliopita wa mavuno chama chetu cha ushirika kiliuza zaidi ya tani 30 za mahindi na tani 60 za maharage kwa sababu WFP ilitusaidia.” 

Immaculee anasema faida anayoipata imemuhamasisha kuwa mkulima stadi na kuzalisha zaidi sio tu kwa ajili ya biashara lakini pia kwa kuhakikisha mlo kwenye familia yake kwani WFP zaidi ya kununua mazao yao inatoa mafunzo, pembejeo na mbegu kwa wakulima. 

Na sasa anawachagiza wanawake wenzie kutobweteka kuingia katika kilimo kwani jembe halimtupi mkulima. 
 

Audio Credit
Grace Kaneiya / Flora Nducha
Audio Duration
2'4"
Photo Credit
UN Food Systems Summit