Endesha baiskeli ujenge afya na kupunguza gharama za maisha
Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya uendeshaji baiskeli duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema uendeshaji baiskeli siyo tu unahifadhi mazingira kwa kupunguza utoaji wa hewa chafuzi za kwenye magari bali pia unapunguza gharama kwa mtumiaji na kujenga afya.