Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Endesha baiskeli ujenge afya na kupunguza gharama za maisha

Endesha baiskeli ujenge afya na kupunguza gharama za maisha

Pakua

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya uendeshaji baiskeli duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema uendeshaji baiskeli siyo tu unahifadhi mazingira kwa kupunguza utoaji wa hewa chafuzi za kwenye magari bali pia unapunguza gharama kwa mtumiaji na kujenga afya. 

Katika kusaka mtazamo wa wananchi kuhusu kauli hiyo, Evarist Mapesa mwandishi wa Radio washirika SAUT FM mkoani Mwanza nchini Tanzania amezungumza na waendesha baiskeli ambao pamoja na mambo mengine wametoa wito kwa kila mtu kujijengea tabia ya kuendesha baiskeli ili kujiepusha na magonjwa nyemelezi. Kwanza akaanza na Thedy Lukanima na kisha Jeremiah Elijah akeleza alivyopokea siku hii 
(Taarifa ya Evarist Mapesa)
 

Audio Credit
Leah Mushi/Evarist Mapesa
Audio Duration
3'53"
Photo Credit
UN-Habitat/Babu Lal