Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais wa Tanzania atoa takwimu za wagonjwa wa COVID-19

Rais wa Tanzania atoa takwimu za wagonjwa wa COVID-19

Pakua

Wakati shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO kanda ya Afrika likionya kuwepo kwa wimbi la tatu la ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 barani Afrika, Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema sasa taifa hilo lina wagonjwa zaidi ya 100 na tayari taratiu zinafanyika ili kuingia chanjo ya COVID-19.
Rais Samia amesema hayo Jumatatu juni 28 2021 wakati akijibu swali wakati wa mkutano wake na wahariri wa vyombo vya habari Ikulu jijini Dar es salaam.

Samia pia ameeleza tayari wameshajiunga na mpango wa Umoja wa Mataifa wa kuchagiza upatikanaji wa chanjo COVAX kwa nchi za kipato cha chini.


Miongoni mwa nchi za Afrika ambako tayari COVAX imewasilisha chanjo ni pamoja na Rwanda, Uganda, Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.
 

Audio Credit
Assumpta/Samia Suluhu Hassa
Audio Duration
2'16"
Photo Credit
© UNICEF Moldova