Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hakuna uzuri wowote wakushiriki ngono katika umri mdogo

Hakuna uzuri wowote wakushiriki ngono katika umri mdogo

Pakua

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto -UNICEF nchini Uganda linafadhili mradi wa Mama kwa Mama ambao unajengea uwezo maafisa wa ustawi wa jamii wanaopita kila kaya maskini kusaka  barubaru na vijana balehe waliopata mimba katika umri mdogo na kuwapatia stadi za ufundi ili  hatimaye waweze kujipatia kipato na kubadilisha maisha yao. 
(Taarifa ya Leah Mushi) 
 
Wilayani Kasese nchini Uganda, video ya shirika la UNICEF inaanza kwa kuonesha binti mwenye umri wa miaka 14 kwa jina la Mary akiwa amembeba mwanae mgongoni na kuni mkononi akiingia ndani ya nyumba yao. Kisha akipuliza moto kupika huku mwanae akiwa gongoni. 
 
Mary sio jina lake halisi. Yeye alipata mimba akiwa kidato cha kwanza kitendo kilicho wahuzunisha sana wazazi wake kwani aliacha shule na kukaa nyumbani. 
 
Maisha yake yaliokolewa na mfanyakazi wa ustawi wa jamii aliyepatiwa mafunzo na UNICEF kupitia mradi wa Mama kwa Mama ili kusaida wasichana wenye madhila kama Mary. Stadi ni pamoja kufuma vikapu, kuoka keki ili wapate fedha za kujikimu. Na ndoto ya kurejea shuleni imerejea… (Sauti ya Mary- Mellissa) 
 "Nataka kurudi shule, sababu nataka kuja kuwa muuguzi ili niwatibu wasichana wengine. Mtoto wangu akiwa mkubwa nataka kurudi shule. " 
 
Na  ujumbe kwa barubaru wengine akisema,… (Sauti ya Mary- Mellissa) 
 "Hakuna uzuri wowote wakushiriki ngono katika umri mdogo kama wetu sababu utapata mimba na ndoto zako zote zitasimama, wenzako watakuwa wanaendelea na shule wakati wewe umekaa nyumbani ukilea mtoto” 
 
Wilaya ya Kasese ina  jumla ya vikundi 47 ambavyo vinatoa ufundi stadi ili kuwapa uwezo mabinti hawa wa kuwa na mwanzo mpya.  
 
Mary nuru imemwangazia tena anafunua madaftari yake ajisomeee maana amepata anarejea shuleni kuendelea na masomo ili aweze kutimiza ndoto yake ya kuwa muuguzi. 
 

Audio Credit
Assumpta Massoi/Leah Mushi
Audio Duration
1'52"
Photo Credit
UNICEF/Henry Bongyereirwe