Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

UNICEF Mozambique/Ricardo Franco

Athari za mabadiliko ya tabianchi ni 'mwiba' kwa watoto- UNICEF

Mwakilishi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, nchini Msumbiji Maria Luisa Fornara akitembelea eneo la Guara Guara ambayo sasa ni makazi ya walioathiriwa na kimbunga Eloise, amesema inasikitisha kuona watoto wakiteseka kwa mara nyingine kutokana na matokeo mabaya ya mabadiliko ya tabianchi.  Grace Kaneiya na maelezo zaidi.

Julius Mwelu/UN-Habitat

Tuchukue hatua sasa kulinda sayari yetu dunia- Ripoti

Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP inatoa muongozo wa jinsi ya kushughulikia changamoto kubwa tatu za dharura zinazoikumba dunia ambazo ni mabadiliko ya tabianchi, kuishi vyema na mazingira na ufikiaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDGs. Jason Nyakundi na maelezo zaidi.

© UNICEF/UNI375881/Ryeng

Baa la njaa lanyemelea Sudan Kusini

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP linasema Sudan Kusini ipo katika hatihati ya baa kubwa la njaa kwani inakabiliwa na viwango vya hali ya juu ya kutokuwa na uhakika wa chakula kuwahi kushuhudiwa tangu taifa hilo changa zaidi duniani kupata uhuru wake yapata miaka 10 iliyopita. Tupate maelezo zaidi na John Kibego

Sauti
3'19"
WHO/Lindsay Mackenzie

Chanjo dhidi ya Ebola DRC yaanza kutolewa eneo ambalo mgonjwa wa kwanza alipatikana

Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO, limeanza kutoa chanjo dhidi ya Ebola kwa wakazi wa eneo la Butembo jimboni Kivu Kaskazini, ikiwa ni wiki moja baada ya mgonjwa mmoja kuthibitishwa kufariki dunia kutokana na ugonjwa huo. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.
(Taarifa ya Assumpta Massoi)
Nats..
Eneo la Butembo katika hospitali ya Matanda, wahudumu wa afya wakiwa wamevalia mavazi yao rasmi ya kujikinga dhidi ya Ebola, ikiwemo barakoa wakijandaa kutoa chanjo dhidi ya gonjwa hilo lililoripotiwa kuibuka tena kwenye jimbo hili la Kivu Kaskazini.

Sauti
3'19"
Vaibhav Gadekar

Mwalimu hajali kipato bali matokeo- Asema mshindi wa tuzo ya mwalimu bora duniani

Mwalimu Ranjitsinh Disale kutoka katika jimbo la Maharashtra ambaye ndiye mshindi wa mwaka wa Tuzo ya kimataifa ya Mwalimu bora duniani kwa mwaka 2020, amesema tuzo ya dola milioni 1 aliyoipata atagawana na washindani wenzake 9 waliofika ngazi ya fainali ili wakaendeleze elimu katika maeneo yao. Taarifa ya Grace Kaneiya inaeleza zaidi. 

Sauti
2'1"
TANZBATT 7/Ibrahim Mayambua

TANZBATT_7 yatamatisha jukumu lao DRC, TANZBATT_8 yapokea kijiti

Kikosi cha 7 cha Tanzania, TANZBATT_7 kwenye kikosi maalum cha kujibu mashambulizi, FIB cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO kimetamatisha jukumu lake rasmi na kukabidhi bendera kwa kikosi cha 8 au TANZBATT_8. Shuhuda wetu kutoka Beni, jimboni Kivu Kaskazini ni Luteni Issa Mwakalambo, afisa habari wa TANZBATT_7. 

Sauti
3'19"
UNICEF/Mike Pflanz

UNHCR na wadau wasaka mamilioni ya fedha kusaidia warundi wanaoishi ukimbizini

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, na wadau wake 33 wametoa ombi la dola milioni 222.6 kuwezesha kusambaza misaada muhimu ya kibinadamu kwa wakimbizi wa Burundi kwa mwaka huu wa 2021. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.

taarifa ya  UNHCR iliyotolewa leo mjini Geneva, Uswisi imesema fedha hizo ni kwa ajili ya wakimbizi wa Burundi ambao kwa takribani miaka saba sasa wanaishi ukimbizini huko Rwanda, Tanzania, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. 

Sauti
2'1"
UNOCHA/Otto Bakano

Hali tete wakimbizi wa ndani nchini Burkina Faso

Dharura kubwa ya kibinadamu inajitokeza nchini Burkina Faso ambapo kuongezeka kwa ukosefu wa usalama na mizozo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita kumesababisha mzozo unaokua kwa kasi zaidi wa makazi, watu zaidi ya milioni wakifurushwa kutoka katika makazi yao. Taarifa ya Ahimidiwe Olotu, inaeleza zaidi. 

Naibu Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA, Ramesh Rajasingham katika ziara yake nchini Burkina Faso amekutana na jamii kadhaa zilizoathiriwa na vurugu na kulazimika kuyakimbia makazi yao. 

Sauti
3'19"
UNMISS/Francesca Mold

UNMISS: Wiki hii tuna mpango wa kutuma walinda amani kote Sudan Kusini.

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, ambaye pia ni mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNMISS, David Shearer, akizungumza na vyombo vya habari katika mji mkuu Juba, ameonya kuwa utekelezaji polepole wa makubaliano ya amani yaliyosainiwa mnamo mwaka 2018 unaleta tishio moja kwa moja kwa amani ambayo tayari ni dhaifu katika taifa hilo jipya zaidi ulimwenguni. John Kibego na maelezo zaidi.

Sauti
2'12"
© UNICEF/Salomon Marie Joseph Beguel

Programu ya UNICEF ya elimu kwa njia ya redio yaokoa watoto wakimbizi Cameroon

Kuelekea siku ya radio duniani tarehe 13 mwezi huu wa Februari, tunakwenda nchini Cameroon ambako mradi wa mafunzo ya elimu kwa njia ya redio yamekuwa jawabu kwa maelfu ya watoto waliofurushwa makwao kutokana na ghasia kwenye maeneo ya kusini-magharibi na kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo.. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.

Mashambulizi katika maeneo ya kusini-magharibi na Kaskazini-magharibi mwa Cameroon yamesababisha maelfu ya watu kukimbia makwao na miongoni mwao ni watoto., hali inayofanya wakose haki yao ya msingi ya elimu.

Sauti
2'1"