Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

UNDP Guatemala/Caroline Trutmann

Kampuni ya Mars na IFAD zachukua hatua kunusuru wakulima wa kakao na walaji wa chokoleti

Mfuko wa kimataifa wa ufadhili wa ajili ya kilimo IFAD na kampuni kubwa ya kutengeneza chokoleti duniani Mars zimeshikamana kuchukua hatua kukabiliana na uhaba wa zao la kakao ambalo ni kiungo muhimu katika utengenezaji wa kiburudisho kinachopendwa kila kona ya dunia, chokoleti. 

Chokoleti moja ya viburudisho vinavyopendwa na watu wengi duniani zinapatikana katika maumbo na mchanganyiko wa kila aina lakini ili ziendelee kutengenezwa zinahitaji kiungo muhimu ambacho ni zao la kakao.

Sauti
2'24"
© UNICEF/UNI322644/Haro

Niger michoro ya mitaani yatumika kuelimisha umma kuhusu COVID-19

Nchini Niger, shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji, IOM kwa kushirikiana na wadau linatumia Sanaa za uchoraji mitaani ili kuelimisha jamii kuhusu jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19. Assumpta Massoi anaarifu zaidi.

Michoro hiyo katika miji ya Agadez, Arlit na mji mkuu Niamey, inafuatia warsha iliyoendeshwa na IOM kwa ushirikiano na shirika la Sanaa ya mitaani bila mipaka, SASF mwaka 2019 ambapo watu zaidi ya 1,000 kutoka Niger peke yake walishiriki.

Sauti
1'49"
TANZBATT 7/Ibrahim Mayambua

TANZBATT 7 yapatia msaada watoto yatima Kivu Kaskazini

Nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC , watoto yatima wa kituo cha New Chance jimboni Kivu Kaskazini, wameshukuru msaada wa hali na mali kutoka kwa walinda amani wa Tanzania. 

Walinda amani kutoka Tanzania, kundi la 7, TANZBATT 7, wanaoongozwa na kamanda wa kikosi Luteni Kanali John Magnus Ndunguru, wanaohudumu katika kikosi cha kujibu mashambulizi, FIB cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC MONUSCO, jimboni Kivu Kaskazini  wanawasili kwenye kituo hiki cha yatima na kutoa misaada yao.

Sauti
1'52"
UNHCR Mauritania

Mauritania, mradi wa UNHCR wasaidia kuleta nuru kwa wakimbizi kutoka Mali

Nchini Mauritania, mradi wa mafunzo ulioendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na wadau wake, umesaidia wakimbizi kutoka Mali kuweza kupata stadi za kujipatia kipato kutunza familia zao na kujiandaa vyema kurejea nyumbani pindi hali itakapokuwa shwari. Assumpta Massoi na taarifa zaidi.

Miongoni mwa wanufaika wa mradi huo ni Farka , mkulima kutoka Niafunke nchini Mali, ambaye ni baba watoto 12 kutoka kwa wake zake wawili.

Sauti
1'43"
© UNICEF/Omar Albam

Baraza la Usalama linachemsha bongo kupata badala, makubaliano ya kuvusha misaada kwenda Syria yakifikia ukomo leo

Leo Julai 10 ndiyo siku ya ukomo wa azimio namba 2504 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaloidhinisha makubaliano ya shughuli za kuvusha misaada ya kibinadamu kupitia mpaka wa Uturuki kuingia Syria. Kutokana na umuhimu wa misaada hiyo, hali hiyo inaweka shinikizo kubwa kwa Baraza la Usalama kutafuta namna ya kuongeza muda zaidi wa uvushaji misaada ili kuokoa maisha ya watu. Taarifa zaidi na Loise Wairimu

Sauti
1'39"
UNICEF/Roger LeMoyne

Kilichotokea Srebrenica yalikuwa mauaji mabaya zaidi Ulaya tangu Vita Kuu ya Pili ya dunia:Guterres

Kuelekea kumbukumbu ya miaka 25 ya mauaji ya kimbari yaliyofanyika huko Srebrenica,Bosnia na Herzegovina, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema huo ulikuwa ukatili mbaya zaidi kufanyika katika ardhi ya Ulaya tangu Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Taarifa zaidi na Jason Nyakundi.

Kupitia ujumbe maalum wa kumbukumbu hiyo ambayo kila mwaka hufanyika Julai 11, Antonio Guterres amesema miaka 25 baada ya mauaji hayo ya kimbari  ya 1995 Umoja wa Mataifa unawaenzi maelfu ya watu waliouawa kikatili na kuahidi kutowasahau asilani.

Sauti
2'23"
UNMISS(Picha ya Maktaba July 2018)

Sudan Kusini yatimiza miaka 9 ya uhuru inachokijua ni vita badala ya amani:UNHCR

Leo ni miaka tisa kamili tangu Sudan Kusini taifa changa kabisa duniani lijinyakulie uhuru baada ya kujitenga na Sudan. Lakini tangu lipate uhuru taifa hilo lilichokishuhudia ni vita zaidi ya amani, wimbi kubwa la wakimbizi na sasa linapambana na janga la corona au COVID-19 kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.

Sauti
1'59"